AJILA, TUME YA UCHAGUZI YATOA NAFASI ZA KAZI YA MUDA

Imewekwa: June 13, 2019
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itaboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, awamu ya kwanza kuanzia mwezi Julai, 2019 kwa kutumia Teknolojia ya kieletroniki ya Biometriki (BVR).
Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Mahakama ya Rufaa), Semistocles Kaijage wakati alipokutana na wakilishi wa Vyama vya Siasa vilivyopata Usajili wa Kudumu katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti, Jaji Semistocles Kaijage alisema kulingana na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Kifungu cha 21 (5), sura 343 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali ya Mitaa Sura ya 292 Tume inapaswa kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mara mbili katika Uchaguzi Mkuu mmoja na Uchaguzi Mkuu mwingine unaofuata.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili utafanyika baada ya kukamilika kwa uboreshaji awamu ya kwanza.
Mhe, Jaji Kaijage alisema kuwa uboreshaji huo unafanyika baada ya kukamilika kwa sehemu kubwa ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari kama uhakiki wa vituo vya kandikisha Wapiga Kura, uandikishaji wa majaribio wa Wapiga Kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, maandalizi ya vifaa vya Uboreshaji wa Daftari na mkakati wa Elimu ya Mpiga Kura.
Mwenyekiti alisema kuwa uandikishaji wa Wapiga Kura wa mwaka huu, 2019 Tume itaandikisha Wapiga Kura wapya na wale waliopoteza kadi za kupigia kura au kadi zao kuharibika, wanaorekebisha taarifa zao na bila kusahau waliohama kutoka maeneo yao ya awali na kuhamia maeneo mengine ya Uchaguzi tofauti na uandikishaji wa mwaka 2015 ambapo wapiga kura wote nchi nzima waliandikishwa.
Ili kuhamasisha wananchi wajitokeze kujiandikisha kwa wingi, Tume itatumia njia mbalimbali za Elimu ya Mpiga Kura kuwaelimisha kupitia Taasisi au Asasi za Kiraia zenye sifa ya kutoa elimu hiyo, kukutana na wananchi ana kwa ana kwa kushiriki maonyesho mbalimbali, mikusanyiko ya kijamii, gari la matangazo la Tume, Vyombo vya Habari, mitandao ya kijamii, Makala za magazeti na machapisho mbalimbali kama mabango na vipeperushi.
Mwenyuekiti pia aliwambia wawakilishi wa Vyama vya siasa kuleta majina ya mawakala wao Tume siku saba kabla ya Uboreshaji ili waapishwe kupata vibali kwa ajili ya kusimamia uandikishaji wa Wapiga Kura vituoni.
Mwaka huu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itakuwa na vituo vya uandikishaji Wapiga Kura 37, 407 tofauti na vituo 36,549 vilivyotumika mwaka 2015 na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) itatumia vituo vya kuandikisha Wapiga Kura 407 tofauti na idadi ya vituo 380 vilivyotumika mwaka 2015.
Aidha, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt. Athumani J. Kihamia alisema kuwa maeneo yanayokubalika kuwekwa vituoa vya uandikishaji Wapiga Kura kulingana na Kanuni ya 12 (2) ya Kanuni za Uboreshaji wa Daftari chini ya Sheria ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kamuni ya 12 (2) ya Kanuni ya Uboreshaji wa Daftari chini ya Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 ni majengo ya umma na maeneo ya wazi yanayofikika kwa urahisi.


Pamoja na hayo, Mkurugenzi wa Uchaguzi alibainisha maeneo yasiyokubalika kwa mujibu wa Kanuni ya 12 (3) ya Kanuni za Uboreshaji wa Daftari ya Sheria ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kanuni ya 15 (3) ya Kanuni za Uboreshaji wa Daftari chini ya Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 ni Kambi za Jeshi, Numba za Ibada na Ofisi za Vyama vya Siasa

Post a Comment

Thanks for visiting negnew.com link with us for more new and popular songs.
we shall be gratigul when you will share to friends and fellows

Previous Post Next Post