HOJA KUU KATIKA MKUTANO WA TCRA, VYOMBO VYA HABARI, JESHI LA POLISI, MAKAMPUNI YA SIMU






Wakubwa Wenzangu naomba nitoe mrejesho wa Mkutano wa tarehe 28/6/2019 ulioitishwa na TCRA pamoja na wadau wengine kanda ya  kati
-Makampuni ya Simu
-Vyombo vya habari
- NIDA
- Jeshi la police
Hakukua na Agenda Maalumu ilikua ni mazungumzo na kubadilishana mawazo
-Mambo yaliyo zungumzwa upande wa makampuni ya simu
1.Mchakato wa kupata loss report mda uongezwe hadi saa 10 badala ya saa 6 mchana police watatoa feedback
2.Freelancer wote wasio waadilifu waondolewe kazini ili kupunguza matukio ya kiharifu kwa kufanya usajili kinyume na utaratibu.
3.Kuna Zile form za utambulisho kwenye kuombea loss report zinatolewa bila maelezo hasa airtel kuna mtu ame observe hicho kitu pale ofisini kwetu.
4.Utoaji wa taarifa za wateja bila idhini yao hasa namba za simu...wanatumiwa bulk sms na baadhi ya taasisi binafsi so wameomba makampuni ya simu au baadhi ya wafanyakaz kuacha kutoa hizo taarifa bila kibali.
5.Taarifa ya Police...Kuna vijana wamekamatwa na kwa sababu ya kupiga magumashi ya usajili kama ifuatavyo
-Kusajili line zaidi ya moja kwa kutumia kitambulisho kimoja na kuziuza kwa waarifu kuna vijana wamekutwa na line zaidi ya 500 na baadhi ya wahalifu wameshakamatwa
-kusajili line zaidi ya moja kwa kumdanganya mteja kua usajili umekataliwa lakini inakua ni njia ya kusajili line zaidi ya moja na kuziuza au kuzidump

Sababu ya kufanya usajili Magumashi kwa maelezo ya Police
1.Wanasajili na kuwauzia waharifu nje ya mkoa hawaziuzi hapa dodoma ndio hizo zinatumika na jamaa wa tuma kwa namba hii
2.Wanasajili line nyingi na hii ndio sababu kubwa ili kujiongezea namba ili waweze kupata bonus hasa ya juu kabisa,so anafyatua namba nyingi na kuziwekea vocha ya 500 ili akidhi vigezo vya bonus hizi line zinauzwa minadani na zingine zinatupya..Na hii wanaifanya wengi na wanaendelea kutajana.

Waliopo Police
Wengi ni vijana wa Voda na Walikamatwa kwa kuwekewa mtego kwenye gate meeting na police kujifanya wateja wa hizo line ,Zaidi ya vijana 20 wa voda wako ndani na baadhi wa Tigo hasa FOS,Airtel hawajapatikana  ila police wanaendelea na kazi yao na vijana wanaendelea kutaja wengine tumepewa angalizo

Zoezi ni Endelevu linaendelea ndani ya dodoma na kuanzia j3 linasambaa kanda nzima..tumepewa angalizo kama kuna vijana wetu wanajihusisha kwenye hayo magumashi sasa hivi atakamatwa kijana na kampuni itahusishwa kwa kumpa kazi kijana ambae hana maadili ya kazi.*

Post a Comment

Thanks for visiting negnew.com link with us for more new and popular songs.
we shall be gratigul when you will share to friends and fellows

Previous Post Next Post